Uongozi wa kuigwa

Aliya İzzetbegoviç ni kiongozi mwenye msimamo na mapenzi ya itikadi ya kiislamu, uchmbuzi wa mkuu wa kitivo cha siasa wa chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt cha Ankara Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL

Uongozi wa kuigwa

Karne ya 20 ni karne ambayo mambo yalikuwa yakienda kombo kwa Waislamu.

Ni karne ambayo waislamu walishuhudia: miji yao  ikivamiwa na kukaliwa kimabavu mmoja baada ya mwingine,  alishuhudia vifo,pamoja na ukandamizwaji wa hali ya juu.

Katika karne hii ambayo uislam ulikuwa  hautakiwi  kabisa ndipo Aliya İzzetbegoviç moja ya watu wachache sana ambae aliwasilisha uzuri wa mawazo na fikra za utamaduni wake wa kiislamu kwa walimwengu. Ni kiongozi ambaye alijitolea maisha yake kupigania fikra za uislamu katika kipindi ambacho uislamu ulikuwa hautazamwi kama mfumo unaotakiwa.

Miaka ya mwanzoni ya Ujana, Miaka ya mwanzo ya kifungo:Uislamu kipindi cha harakati za miladia

Aliya İzzetbegoviç ni jina ambalo alilirithi kutoka kwa babu yake, alizaliwa mwaka 1925, alipata mafunzo ya kijeshi Istanbul/ Üsküdar kipindi hicho cha mafunzo ya jeshi alimuoa binti wa kituruki mjukuu wa mama Siddika. Labda ndio kwasababu hii nikiwa maeneo ya Aliya na na mitaa ya Üsküdar mjini Istanbul nahisi vitu vinavyo fanana kihistoria, utulivu, busara, ukomavu na ushindi vitu ambavyo vinatoka mbali sana katika historia.

Muda ambao alizaliwa na ujana wake wa mwanzo ni muda ambao historia ya dunia ilikuwa inapitia kipindi kigumu cha migogoro mikubwa. Ni miaka ya mwisho wa vita kuu ya kwanza ya dunia na ya vita kuu ya pili ya dunia .

Kwa kawaida miaka hio ni miaka iliyokuwa ya mateso makubwa kwa waislam haswaa waislamu wa maeneo ya balkani. Baada ya vita ya pili ya dunia , magharibi ndio walioshinda vita hii dhidi ya ufashisti na unazi wa kina Stalin wa Umoja wa Sovieti wa kipindi hicho ambao pia walikuwa ni wakomunisti.

. Baada ya Utawala wa Ottoman, ambao ulikuwa umedumu kwa miaka 200 katika mataifa haya ya Balkani, kuanguka. Mataifa haya hayakutazama tena Uislamu kama njia mbadala ya kuendesha maisha yao ya kila siku.

Ni kipindi hichi ndipo Aliya   akiwa miaka yake ya mwanzo wa sekondari ya upili alipoanzisha vuguvugu la kuhuisha upya uislamu miongoni mwa vijana vuguvugu hilo lilijulikana kama “Mladi Müslümani”  .

Vuguvugu hili ambalo kwa upande mmoja lengo lake lilikuwa kuwafundisha watu elimu ya Uislamu kwa upande mwingine ilikuwa na  lengo la kuwasaidia watu kuponyesha majeraha yao na madhalimu waliyopitia wakati wa vita. Juhudi hizi hazikupendwa na viongozi wa kikomunisti waliokuwako eneo hili hivyo basi ilipelekea Aliya kufungwa kifungo cha miaka mitano gerezani akiwa bado kijana mdogo.

Aliya baina ya mashariki na magharibi

Baada ya kifungo Aliya aliendelea na harakati zake za kutetea maslahi ya jamii na utu kwa ujumla.  Kwa upande mmoja akiwa anataka kujiweka mbali na ujinga uliokuwa umekubuhu kwenye jamii yake kipindi hicho upande mwingine alikuwa anataka awe na elimu mpya zaidi. “Uislamu kati ya mashariki na magharibi” ni moja ya kazi ya Aliya inayoonyesha mtizamo wake mpana juu ya uislamu.

Katika kazi hii amekosoa pande zote mbili mashariki na magharibi. “Nikienda Ulaya siwi mnyonge kwa kuwa  sisi hatukuuwa watoto, wanawake wala vikongwe, wala hatukushambulia maeneo matakatifu. Vitu ambavyo wenzetu wa magharibi wamevifanya, tena wakiwa na fikra kwamba kufanya hivyo ni kwa  ajili ya kukuza ustaarabu wao”.

Kwa mujibu wa Aliya matatizo makubwa ya waislamu ni kutoelewana wao kwa wao, kutokuwa na elimu, kutofanya yale wanayoyasema. “Uislamu ni jina la kila kitu kizuri na cha asili” kwa mtazamo wangu, maneno haya ya Aliya ni wito kwa waislamu wote wapambane na matatizo haya. “Uislamu ni kuwa mbora katika kila kitu”.

Lakini sisi waislamu sio wabora. Mara nyingi tunachanganya haya mambo mawili tofauti.

“ Ili uwe mwalimu  katika uso wa  ardhi inabidi uwe mwanafunzi katika uso wa mbingu”

Miaka ya vita...

Aliya alijikuta akienda jela tena  kipindi ,hiki ikiwa ni miaka 14, kutokana na kitabu chake alichokiita “Islamic manifesto”, tukio hili lilitokea kabla mataifa ya  Balkani hayajagawanyika kwa mara nyingine. Aliya alipata msamaha na kuachiwa huru mnamo mwaka1988 baada ya kuwa ametumikia kifungo kwa miaka 5. Mwaka 1990 alianzisha chama cha kidemokrasia “ Party of democratic action”.

Baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika kipindi hicho Aliya akachaguliwa kuwa rais wa kwanza wa nchi yake. Mwaka 1992 Boznia Hazegovina ilipata uhuru wake toka kwa Yugoslavia. Mataifa ya magharibi yalizisaidia nchi za Crotia na Slovenia katika harakati zao za kudai uhuru, Lakini kutokana na unafiki mkubwa wa mataifa haya ya magharibi waliacha vita kali ya Bosnia iendelee, na kufanya dunia kushuhudia umwagaji wa damu mkubwa na mauaji ya halaiki katika karne ya 20.

Ni miaka hiyo ya vita ndipo dunia ikamtambua Aliya kama kiongozi. Pamoja na umaskini mkubwa, vikwazo vya kiuchumi Aliya hakurudi juma, alidumu katika misimamo yake ya kukumbatia fikra za kiisalamu, Aliionyesha dunia na waislamu jinsi inavyowezekana kupinga dhulma na udhalimu, bila kukata tamaa hata kama ukiwa mnyonge.

Vitendo walivyokuwa wanafanya Waserbia kuwaadhibu watu waliokuwa wanapinga udhalimu kwa kuwaua watoto, wanawake na wazee wa kiboznia, imekuwa ndio sheria kubwa ya vita.

 “Maadui zetu wanatudai kitu kimoja tu: Haki”

“Waserbia sio waalimu wetu”

“kushindwa haswaa sio kushindwa vita isipokuwa, kufanana na adui kimatendo ”

Wakati wa vita mwanahabari mjerumani alimuuliza Aliya “ Dhulma zote hizo mlizofanyiwa  kwa nini  usiamrishe watu wako walipize kisasi” Majibu yake na matendo yake ni moja ya vitu vinavyoonyesha fikra zake za kiislamu na ukubwa wake, alisema “ Kitabu ninachokiamini hakiniruhusu kufanya hayo”

Kama hivi sasa nchini bosnia fikra za Aliya zikiwa hazitiliwi maanani tena, haitokani na kwamba fikra hizo zilikuwa na walakini au Labda Aliya  hakutosha bali inatokana na kwamba dunia hii inayoongozwa na Marekani kutoridhika kuona jamii ya waislamu katikati ya Ulaya ikimea na kustawi.

Urithi…

 “Walituzika udongoni.Ambacho hawakujua ni kwamba sisi tulikuwa mbegu” inasemekana maneno haya aliyasema Aliya kuwaambia wana Balkan.

Maneno haya yana jumuisha historia ya miaka 200 ya Waislamu. Miaka 200 ya kutojibu mapigo, kipindi cha kurudi nyuma. Kwabahati mbaya viongozi wa mfano wa Aliya ni wachache sana

Kama ilivyokuwa kwenye makalayetu iliyopita ya “tujipange vipi kukabiliana na wamagharibi” lengo halikuwa kupinga au kukubaliana na hoja fulani bali kuchagiza ubongo ufikirie kwa kina na kwa undani juu ya aina ya viongozi ambao wanaona mbali na wanoweza kutupatia ufumbuzi wa matatizo yetu. Viongozi kama Aliya, Said Halim Paşa, Iqbal, Akif, Rashid al-Ghannouchi, ni katika viongozi wachache sana wa zama hizi ambao walilenga kufikisha itikadi ya kiislamu.

Pamoja na kuwa alikandamizwa, akadhulumiwa na kufanyiwa kila aina ya vitimbi, ujumbe wake ulikuwa ni viongozi ambao maono yao hayazidi kabila, nchi au jamii anayotoka hawana cha kuzipa jamii.

Kiongozi kama Aliya ambae pamoja na dhulma alizopitia, hakulipiza kwa dhulma na chuki bali kwa itikadi yake  na fikra zake za  Uislamu, kwa elimu, kwa hekma kwa ukarimu na upendo.

Kiongozi ambaye anataka atende haki katika kila jambo  sio tu waislamu ndo wanaomuhitaji bali dunia nzima inahitaji viongozi wa aina hii.

Mkuu wa kitivo cha siasa wa chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt cha Ankara Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL anafafanua...Habari Zinazohusiana