BASATA yashusha kibano kwa Rayvan na Diamond Tanzania

Baraza la Sanaa la Tanzania limeufungia wimbo mpya wa Rayvan akimshirikisha Diamond, pamoja na kuwatoza faini wasanii hao kwa kukiuka maadili

BASATA yashusha kibano kwa  Rayvan na Diamond Tanzania

Baraza la Sanaa la Tanzania ,BASATA , limeufungia wimbo mpya wa msanii Rayvanny aliomshirikisha Diamond  uitwao "Mwanza" kutokana na kile ambacho kimetajwa kuwa  kukiuka maadili.

Wasanii hao pia wametozwa faini ya  milioni tatu sarafu ya Tanzania Shilingi kila mmoja.

Lebo ya muziki inayowasimamia wasanii hao pia imetozwa faini ya shilingi milioni tatu.

Taarifa hiyo  himetolewa na katibu wa baraza hilo, Geofrey Muingereza alipozungumza na wanahabari.Habari Zinazohusiana