Wanasayansi wa Kituruki wapata tuzo ya juu nchini Marekani

Nurcin Celik wa chuo kikuu cha Miami na Sinan Keten wa chuo cha Northwestern watunukiwa tuzo ya juu na Barack Obama

Wanasayansi wa Kituruki wapata tuzo ya juu nchini Marekani

Rais Barack Obama awatunuku wanasayansi wawili kutoka Uturuki tuzo ya juu ya Marekani kwa heshima ya utaalamu wao katika kitengo cha uhandisi .

Obama alitoa tuzo hizo kwa Nurcin Celik wa chuo kikuu cha Miami na Sinan Keten wa chuo kikuu cha Northwestern.

Obama alisema kuwa anawapongeza wanasayansi hao kwa kazi yao ya matokeo mazuri katika uhandisi .

Obama alikuwa anatoa hotuba katika hafla ya kutoa tuzo kwa wanasayansi na watafiti 102 waliofanikiwa katika kazi zao.

Nurcin Celik alisomea katika chuo kikuu cha Bosphorus jijini Istanbul na kuhitimu kisha baadaye kuendelea na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Arizona ambapo alisomea uhandisi wa viwanda  na kumaliza PHD katika chuo hicho mnamo 2010.

Keten naye pia alisomea katika chuo kikuu cha Bosphorus,baadaye aliendelea na uzamili kitengo cha uhandisi katika taasisi ya teknolojia ya Massachusetts  na mwisho kufanya PHD katika chuo hicho hicho.

 Habari Zinazohusiana