Uturuki yashirikiana na Uzbekistan kwenye sekta ya afya

Ujumbe kutoka Uturuki unajumuisha madaktari 15 ambao watafanyia upasuaji zaidi ya watoto 130

Uturuki yashirikiana na Uzbekistan kwenye sekta ya afya

 

Imeanzishwa wiki ya afya baina ya  Uturuki na Uzbekistan, jumatatu katika jiji la Termez, kusini kusini mwa Uzbekistan.

Tukio hili ni sehemu ya ushirikiano kati ya wizara za afya za Uturuki na Uzbekistan, Shirika la ushirikiano na misaada la Uturuki (TIKA), na shirika la afya la Uzbekistan.

Ujumbe kutoka Uturuki unajumuisha madaktari 15 ambao watafanyia upasuaji zaidi ya watoto 130, wanaolazwa kwenye hospitali ya watoto ya mji wa Termez, hadi 6 Oktoba.

Watoto wote hao watapata matibabu bila malipo.

Vifaa vyote vya matibabu, na dawa ni gharama ya serekali ya Uturuki.

Madaktari wa Uturuki watashirikiana na wenzao wa Uzbekistan wakati wa zoezi hili.Habari Zinazohusiana