Atolewa figo kwa bahati mbaya Ujerumani

Kijana mwenye asili ya kituruki ametolewa figo kwa bahati mbaya wakati wa upasuaji katika moja ya hospitali nchini Ujerumani.

Atolewa figo kwa bahati mbaya Ujerumani

Kijana mwenye asili ya kituruki ametolewa figo kwa bahati mbaya wakati wa upasuaji katika moja ya hospitali nchini Ujerumani.

Kwa mujibu wa habari,kijana huyo Kerim Ramazan Ucar mwenye umri wa miaka 18 alienda hospitali kwa nia ya kufanyiwa upasuaji wa bandama lakini madaktari wakafanya makosa makubwa na kumtoa figo yake moja.

Kijana huyo aliyekuwa na ndoto za kuwa mwanariadha amepigwa na bumbuazi baada ya kupewa ripoti kuwa ametolewa figo kwa bahati mbaya.

Ripoti zinaonyesha kuwa daktari aliyemfanyia upasuaji ana uzoefu wa miaka thelathini na tano na mpaka sasa hajatoa tamko lolote kuhusiana na makosa hayo.

Kijana huyo anasema kuwa alijiskia mchovu na kuumwa sana baada ya kufanyiwa upasuaji huo.

Familia ya Kerim imewataka polisi kuingilia kati kwani kosa hilo limekuwa la kipuuzi sana,toka lini bandama ikachanganywa na figo?Habari Zinazohusiana