Ndege ya kwanza ya kivita ya Uturuki aina ya F-35

Wiki kadhaa za kutolewa kwa ndege za kivita aina ya F-35  za Uturuki

Ndege ya kwanza ya kivita ya Uturuki aina ya F-35

 

Naibu  mkurugenzi katika kitengo cha utafiti wa teknolojia ya kisasa amepeperusha   video katika ukurasa wake wa Twitter ikionesha  ndege ya kivita aina ya F-35 ikiwa na  bendera ya Uturuki. 

Ndege hiyo ya kivita ya Uturuki imeonekana katika kambi ya Lockheed Texas ikiwa angani ikiwa na bendera ya Uturuki.

Ndege ya kwanza aina ya F-35 ya jeshi la Uturuki imeandaliwa kufanyiwa  hafla maalumu ifikapo Juni 21 mwaka 2018 Marekani.

Baada ya mazoezi kwa marubani wa ndege hizo za kivita, ndege hiyo itapelekwa katika  kambi ya Malatya Uturuki.
 Ndege ya kivita aina ya F-35 inatarajiwa kuanza kuruka katika anga la Uturuki  mwaka 2019.

 

 Habari Zinazohusiana