Gari la kivita lisilokuwa na dereva UKAP lipo tayari

Gari la kivita la Uturuki lisilokuwa na dereva  UKAP lipo  tayari

Gari la kivita lisilokuwa na dereva UKAP lipo tayari


Mashirika ya Uturuki katikka idara ya ulinzi kwa ushirikiano yanaonesha maendeleo kwa kuunda gari jipya la kivita lisilokuwa na dereva.

Mashirika hayo kwa pamoja  yameonesha uwezo wake  wa uzalishji katika teknolojia ya kisasa.

UKAP imefanyiwa utafiti na  na shirika la  kienektroniki la Uturuki na shirika la silaha za kisasa  ASELSAN. Baada ya majaribio  , jeshi limetangaza kuwa gari lipo tayari kuanza kazi.

Majaribio ya gari hilo yamefanyiwa katika maeneo tofauti ambayo  yanakwenda na hali halisi katika maeneo magumu na yenye vizuizi.
 
Gari hilo  litakuwa na uwezo wa  kufanya kazi bila ya kuhariba katika maeneo ya joto kali. Magari hayo yatakuwa yakichangia  kuimarisha usalama katika maeneo tofauti.

Gari hilo litaoneshwa katika maonesho ya magari ya kivita mjini Paris nchini Ufaransa baina ya Juni 11 na Juni 15. Maonesho hayo yatakuwa maonesho ya Eurosatory.Habari Zinazohusiana