Uzalishaji wa viwanda nchini Uturuki waongezeka kwa 10.4% mwezi Septemba

Takwimu zinaonyesha kuwa uzalishaji wa viwanda nchini Uturuki uliongezeka kwa asilimia 10.4 mwezi Septemba, ikilinganishwa na kipindi hicho cha mwaka 2016.

Taasisi ya Uturuki ya Takwimu (TUIK) ilİtoa Jumatano takwimu za uzalishaji wa viwanda nchini Uturuki wa mwezi Septemba 2017.

Kwa mujibu wa TUIK, ripoti ya uzalishaji wa viwanda iliorekebishwa imeonesha ongezeka la asilimia 10.4 Septemba 2017, ikilinganishwa na mwezi huo huo wa mwaka uliopita.

Hata hivyo, takwimu za Septemba 2017 zimeonesha upungufu wa 0.4% ikilinganishwa na Agosti 2017.

Wanauchumi ambao walishiriki katika Utafiti wa Uzalishaji wa Viwanda, ulioandaliwa na Kituo cha Fedha cha Anadolu (AA) , walitabiri ongezeko la asilimia 10.5 mwezi Septemba, kabla ya ripoti kufanyiwa marekebisho, ikilinganishwa na mwezi huo huo mwaka uliopita.Habari Zinazohusiana