Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Haberturk : « Maelewano ya ushirikiano wa kisiasa »

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan rais wa Urusi Vladimir Putin  wamekutana Sotchi na kuzungumzia kuhusu hali inayoendelea nchini Syria. Viongozi hao wawili walikuwa wakizungumzia  kuhusu mzozo wa Syria ambao tayari umedumu kwa mrefu. Rais Erdoğan amesema kuwa katika mazzungumzo yao na rais Putin wamekubaliana na kutafuta suluhu kuhusu mzozo wa Syria kwa njia kisiasa. Rais Putin amemuunga mkono  harakati na juhudi katika kutafuta suluhu katika mzozo wa Syria.

Star : « Waziri mkuu wa Uturuki afanya mazungumzo kwa njia ya simu na naibu wa Iran Jahangiri »

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım amefahamisha kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na naibu wa Iran Jhangari. Waziri mkuu wa Uturuki imetoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea Jumapili usiku katika mpaka wa Iraq na İran.  Kwa mujibu wa taarifa zilzitolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Uturuki, Uturuki itashirikiana na  na Iran kwa hali na mali katika kipindi hiki cha majınzi baada ya tetemeko la ardhi. Jahangiri kwa upande wake pia  ametoa shukrani kwa  Uturuki kwa kujitolea kwake.

Hurriyet : « Mataifa yatakayo ongozwa mwaka 2050 , Uturuki imo ...»

Mataifa yatakayo ongoza ulimwengu mwaka 2050 Uturuki pia yaonekana kupiku baadhi ya mataifa makubwa. Shirika la takwimu la  PriceWaterhouseCoopers (PWC) limetoa makala ambayo inakadiria mataifa ambayo yanatarajiwa kuwa mataifa makubwa ifikapo mwaka 2050. Katika orodha yake shirika hilo  limesema kuwa Uturuki  itapiku  mataifa ya Ulaya  kwa mabadiliko  makubwa. Uturuki itachukuwa nafasi ya 10 ifikapo mwaka 2050.    Kutoka na  kushuka kwa uchumi barani Ulaya na  sheria kuhusu mzazi  kutalifanya bara la Ulaya kudhoofika ifikapo mwaka 2050.

Vatan : « Urithi wa Atatürk »

Mashua ya Kartal II , mashua ambayo alikuemo baba wa taifa la Uturuki  Mustafa Kemal Atatürk wakati kunatolewa ishara ya kwanza  ya vita vya ukombozi imekuwa moja ya majumba ya makumbusho. Mustafa Kemal Atatürk alisema katika mashua hiyo kuwa wanaotaka kuikalia Uturuki wataondoka kama walivyokuja Novemba 13 mwaka 1918 Bosphorus. 

 


Tagi: Uturuki

Habari Zinazohusiana