Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia,mji wa Ephesus

Hikaya za Anatolia

Leo katika kipindi Chetu cha hadithi za Anatolia, tunawaletea kisa kikubwa cha mama wa Yesu,Maryam ambaye inasadikika kwamba nyumba yake ilikuepo katika mji wa Efes. Takriban miaka 2000 iliyopita, Mji wa Efes uliaminika kuwa  mji ambao ulikua na wakazi wangi kupita miji mingine yote iliyopo Anatolia. Ulikua na jumla ya wakazi laki 2. Baada ya Kuondoka Nabii Isa, wanafunzi wake waliamua kumhamisha  Mama Maryam na kumpeleka katika mji wa Efes wakipitia sehemu mbalimbali kama vile,Syria na Antiyok. Inasadikika kuwa Mama Maryam alifariki katika mji huu baada ya kuishi kwa miaka takriban 9. Baada ya Kufariki, sehemu aliyoishi ikasahaulika na kupotea. Mama Maryam ni mtu mkuu na mtukufu  kwa Waislam na Wakristu. Anakubalika katika dini zote mbili kuwa yeye ndiye mama wa nabii Isa.  Hata sura mojawapo ya Quran tukufu imepewa jina la Maryam na inamuelezea utukufu wake. 

 

Inapita miaka Mingi na watu wa Anatolia wanasahau kwamba Mama Maryam aliishi katika Mji wa Efes na kukata pumzi yake ya mwisho akiwa hapo. Siku moja, mwanamke mwenye asilia ya Kijerumani,aliyekua mgonjwa kwa kipindi kirefu alianza kupata maono ya dini. Ingawa alielezea kwa kina aloyoyaona katika ndoto, lakin watu hawakumuamin. Mshairi mmoja maarufu aliyejulikana kama Brentano  alirekodi maelezo yake na kuchapisha kitabu baada ya kifo chake mnamo mwaka 1842. Muda mrefu tena ukapita baada ya kutolewa kitabu hiki.  Kitabu kikawafikia Wakristu waishio mjini Izmir. Kikaanza kusomwa na kuleta mijadala makanisani. Kiongozi mmoja wa kanisa ambaye asla hakukubali uwepo wa kaburi la Mama Maryam katika eneo la Anatolia, akaamua kuunda kikundi na kukituma Efes kwa ajili ya kuchunguza mnamo mwaka 1891. Ingawa walikwenda kwa shida,lakin walifanikiwa kufika mjini Efes. Wakakuta magofu ya kanisa na nyumba ambayo Mama Maryam aliishi miaka ya nyuma katika namna ileile aliyoielezea mwanamke wa Kijerumani. Habari hii ikamfikia Papa ndani ya muda mfupi. Mji huu wa kihistoria umekua ni sehemu ambayo Wakristu wangi humiminika kuja kuzuru sehemu aliyoishi mama Maryam na Waislam nao hawapungui kuitembelea. 

Siku ukipata wasaa wa kuitembelea Anadolu, usikose kufika maeneo haya ya milima ya Bülbül ili ujionee alipoishi mama yetu mtukufu. 

Tukutane tena Juma lijalo kwa kipindi kingine maridhawa cha Hadithi za AnatoliaHabari Zinazohusiana