Uchambuzi wa Matukio

Mapambano ya Uturuki dhidi ya ugaidi

Uchambuzi wa Matukio

Uturuki inapambana na ugaidi kwa moyo mmoja tangu miaka30 iliopita ya historia ya uUturuki.

Katika kipindi hicho cha miaka zaidi ya 30, mamaia ya raia  yamepoteza maisha yao kutokana na matendo ya kigaidi  ya kundi la wanamgambo wa PKK na kusababisha pia uharibifu mkubwa mali.

Zaidi ya janga la ugaidi wa kundi la kigaidi la PKK, Uturuki imejipata pia katika uhalifu unaosababishwa na kundi la wanamgambo wa Daesh ambapo mizizi yake ilianza kumea nchini Syria na Irak kutoka na hali mbaya ilikuwa ikijiri katika mataifa hayo kutokana  na  mapigano yasikuwa na mwisho.

Hali hiyo ilipelekea Uturuki kuchukuwa uamuzi wake wa kupambana na kundi la Daesh pamoja na kundi la wanamgambo wa PKK.

Kwa ujumla Uturuki  imefaanikiwa kupunguza uhalifu unasababishwa na wanamgambo wa makundi hayo katika ardhi yake.

Uturuki ililazimikwa kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi katika mipaka yake  na kuhakikisha kuondoa vitisho vya magaidi katika mipaka yake.

Uturuki ilianzisha mapambano dhidi ya kundi la PKK na Daesh  kutokana na kwamba makundi hayo yalikuwa tayari yameweka ngome zake  katika maeneo yaliopo mpakani mwa Uturuki kwa kuwa kulikuwa hakuna usalama katika eneo hilo.

Makundi ya kigaidi yalifaulu kuweka ngome zao katika eneo la mpakani mwa Uturuki na Syria.

Uturuki na jeshi lake lenye nguvu liliwaondoa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh  katika operesheni yake ilijulikana kwa jina la operesheni ya Efratia na operesheni nyingine ya Tawi la Mzaituni ilioanzishwa kwa lengo la kuwaondoa wanamgambo wa kundi la PYD ambalo ni tawi la kundi la kigaidi la PKK nchini Syria.

Kundi la wanamgambo wa YPG  wapo Afrin kwa  muda wa miaka kadhaa. Uwepo wa wanamgambo wa kundi hilo unatishia usalama wa Uturuki.

Wanamgambo hao hujaribu mara kwa mara  kupenyeza sialaha kutoka Afrin na hadi Uturuki. Wanamgambo hao hutumia  milima ya Amanos. Ni wazi kuwa  wanamgambo hao ni tishi kwa usalama wa Uturuki.

Jeshi la Uturuki lilifaulu kukamata silaha zilizopenyezwa na wanamgambo hao katika ardhi ya Uturuki katika operesheni zake zilizokuwa zikiendeshwa dhidi ya ugaidi.

Uwepo pia wa wanamgambo wa kundi la YPG Afrin ulipelekea  kushirikiana na wanamagmbo wa kundi la PKK.

Wanamgambo hao  wameshawishi kwa mbinu tofauti kujipatia wafuasi kupitia propaganda  na kulifanya kundi la PKK kuwa na wanachama wengi.

Raia wengi waliuawa na wanamgambo wa kundi la YPG katika maeneo kama  Kilis na Reyhanli. Iwapo operesheni ya Tawi la Mzaituni itamalizika kwa ushindia unaoonekana  wanamagmbo wa kundi la YPG Afrin operesheni hiyo itaondoa matumaini ya wanamgambo wa kundi la PK.

Wanamgambo wa kundi hilo walikuwa na lengo la kuwelka ngome zao katika eneo Kusini mwa Uturuki mpakani mwa Uturuki kwenda Irak hadi katika bahari ya Mediterania.

Eneo ambalo lilikuwa likialiwa na wanmagmbo wa kundi la kigaidi la PYD sio tishio pekee kwa Uturuki bali tishio kwa usalama wa eneo zima na Syria.

Uongozi wa KCK ambao unashirikiana na kundi la YPG  haujaacha ndoto zake za kutakuwa na eneo huru kwa jamii ya wakuridi katika ardhi ya Syria , Iran , Irak na Uturuki.

Ramani iliokuwa na mpango huo ilikutwa katika eneo lililosafishwa na kuondoa vitisho vya wanamgambo wa YPG Afrin katika operesheni.

Katika eneo lilikuwa lipo chini ya wanamgambo wa YPG , kundi hilo lilijaru kuandaa uchaguzi Kaskazini mwa Syria.

Operehsni ya jeshi la Uturuki Afrin ina lengo la kuwaondoa wanamgambo wa kundi hilo la YPG  na kuwanusuru raia na unyama wa wanamgambo wa kundi hilo. Kama tunavyofahamu raia wengi Afrin  ni jamii ya wakurdi wa Syria.

Mamia ya wakurdi walikimbia unyama na uhalifu wa YPG  kuelekea Uturuki, Irak na baadhi ya mataifa ya Ulaya.

Nchini Uturuki kuna zaidi ya  wakurdi kutoka Syria 300 000 ambao ni wazi kuwa wamekimbia  uhalifu wa YPG.

Tunafahamu kuwa  jamii ya wakurdi  wa Syria ilioko Afrin na inaitaji kuondoka ila wanajipata katika mtengo wa kundi la YPG  linalowazuia kuondoka katika eneo hilo.

Jeshi la Uturuki limeendesha operesheni ya Afrin kwa malengo tofauti kama kuondoa vitisho vya kigaidi katika mipaka yake na Syria, kuwaondoa wanamgambo wa YPG Afrin  na kuondoa vitisho vinavyuowakabila raia wa jamii ya kikurdi Syria .

Vitisho vya wanamgambo wa kundi la Daesh  Uturuki vitaondolewa moja kwa moja  baada ya opereshni hiyo na kuwaondoa wanamgambo wa YPG mpakani mwa Uturuki na Syria.

Operesheni ya Tawi la Mzaituni  inadhoofisha ushawishi wa kundi la PKK/PYD katika ukanda.

Wakaazi wa  Manbij, Hasake , Rakka na Deir Ez Zor tayari wameanza  kuonesha kuchoshwa na vitendo vya ugaidi vya YPG.

Mataifa kama Marekani yanayotoa  usaidizi kwa magaidi  yatapata athari  ya jambo hilo.Habari Zinazohusiana