Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Sabah : « Erdoğan : 'Damu za wapalestina katika mikono ya Nyakatahu'…

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan ametuma ujumbe wa Twitter kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Katika ujumbe huo rais Erdoğan amemshutumu waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa kiongozi wa taifa la kibaguzi na lenye kuua watu wasio na hatia. “Kuna damu ya wapalestina katika mikono yako”,aliandika rais Erdoğan. Rais Erdoğan ameongeza kwa kusema kuwa  Netanyahu ni waziri wa taifa lililokalia kimabavu ardhi ya wapalestina kwa zaidi ya miaka sitini.

Hurriyet : « Pigo kwa mchakato wa amani…

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım asema kuwa kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani kutoka mjini Tel Aviv na kuhamishiwa mjini Yerusalemu  ni pigo kwa mchakato wa amani Mashariki ya Kati baina ya Israel na Palestina. Uamuzi huo uliochukuliwa na Marekani kufungua ubalozi wake mjini Yerusalemu haina maana yeyote  bali kuvuruga amani.  Ufunguzi wa ubalozi  wa Marekani Yerusalemu  ni siku ya kihistoria  ambayo damu za wapalestina zimemwagika wikitetea haki yao. Tunalaani  matumizi ya nguvu na ubabe wanaotendewa wapalestina amesema waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım.

Star: «Rais wa zamani wa Tunisia: 'Mataifa ya kiarabu yachukulie mfano Uturuki kuhusu Yerusalemu '…

Rais wa zamani wa Tunisia Moncef Marzuki a ametoa pongezi kwa rais wa Uturuki Rece Tayyıp Erdoğan akiwa mjini Istanbul  kwa msimamo kuhusu suala zima la Yerusalemu.  Rais huyo wa zamani wa Tunisia ametoa wito kwa mataifa ya kiarabu  kuwa angalau na msimamu kuhusu Yerusalemu na kuchulia mfano Uturuki na uongozi wa rais Erdoğan.

Vatan: « Wanaendelea kuwasili Uturuki...

Shirika la watalii la Urusi Rosturizm limefahamisha kuwa watalii kutoka nchini Urusi wanaendelea kumiminika nchini Uturuki. Uturuki imechaguliwa na raia wa Urusi wenye kupenda kutalii mwaka 2018. Tangu mwanzoni mwa mwezi Mei watalii kutoka nchini Urusi wameongezeka nchini Uturuki. Asilimia 52,3.

 Habari Zinazohusiana