Rais Erdoğan asifu jitihada za jeshi la Polisi dhidi ya ugaidi

Rais Erdoğan amemwaga sifa kwa polisi nchini Uturuki kwa jitihada zao madhubuti katika kuhakikisha nchi inapambana na ugaidi.

Rais Erdoğan asifu jitihada za jeshi la Polisi dhidi ya ugaidi

Rais Erdoğan amemwaga sifa kwa jeshi la  Polisi nchini Uturuki kwa jitihada zao madhubuti katika kuhakikisha nchi inapambana na ugaidi.

Hayo rais Erdoğan ameyazungumza wakati wa iftar mjini Istanbul.

"Nasema wazi kuwa ni nchi chache zenye uwezo wa kupambana kwa haki na kundi lenye mizizi mirefu kama FETÖ",alisema Erdoğan.

"Ni watu wachache ulimwenguni wanaweza kutatua janga hili kama vile watu wetu walivyofanya",aliongeza rais Erdoğan.

Kundi la FETÖ ndilo linashutumiwa kujihusisha na jaribio la mapinduzi la 15 Julai 2016.

Jaribio hilo lilisababisha vifo vya watu  250 na majeruhi 2,200.

 Habari Zinazohusiana