Uongozi wa masuala ya kidini wa Uturuki wakemea uamuzi wa Austria kufunga miskiti

bDiyanet, uongozi wa masuala ya kidini wa Uturuki wakemea uamuzi wa serikali ya Austria kufunga miskiti na kuwafukuza maimamu kadhaa nchini humo

Uongozi wa masuala ya kidini wa Uturuki wakemea  uamuzi wa Austria  kufunga miskiti

Uongozi wa masuala ya kidini wa Uturuki Diyanet wakemea uamuzi wa serikali ya Austria kufunga miskiti 7 na kufahamisha kuwa viongozi kadhaa wa dini ya uislamu watafukuzwa kutoka katika taifa hilo.

Miongoni mwa miskiti ambayo imefungwa na serikali ya Austria,   umo mskiti mmoja ambao unashirikiana na Uturuki.

Kwa upande wake kiongozi wa masuala ya kiislamu Ali Erbaş amesema kuwa kitendo hicho cha miskiti kufungwa ni kitendo cha kulaaniwa.

Ali Erbaş amesema hayo katika hotuba yake aliotoa katika mkoa wa Ordu Kaskazini mwa Uturuki aliipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Ali Erbaş ameendelea kusema kwamba uamuzi huo ni kinyume na uhuru wa kuabudu na haki za binadamu.

 Habari Zinazohusiana