Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Hürriyet : « Waziri mkuu wa Uturuki na uamuzi wa Marekani kuhusu ndege za F-35 »

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım azungumzia kuhusu uamuzi wa Marekani kutaka kuzuia Uturuki kununua ndege ainaya F-35 kutoka Marekani. Waziri mkuu wa Uturuki amesema kuwa  kuzuia Uturuki kununua ndege hizo ni kinyume  na sheria kwa kuwa Uturuki ni mshirika wa kimkakati.

Star : « Iran yaiunga mkono Uturuki »

Mohammed Jawad Jemali Nubendegani, mwanachama wa kamishna ya usalama  wa taşfa  na siara  katika baraza la bunge la Iran  amefahamisha kuwa Iran inaunga mkono harakati za Uturuki za kupambana   na ugaidi na ugaidi wa  kundi la PKK.

Sabah : « utalii wapamba moto Trabzon »

Idadi ya watalii yazidi kuongezeka  Trabzon tangu mwanzoni mwa mwaka 2018. Watalii wengi wanatoka ktika mataifa ya Ghuba . Idadi ya watalii imefikia watu 100 000 mkoani Trabzon. Nyumba za wageni  zimekodishwa kwa asilimia 80.

Yeni Şafak : « Thailand na treni ya chini ya ardhi kutoka Uturuki »

Uturuki  na treni ya kwanza ya kupita  chini ya ardhi nchini Thailand. Treni 22  ambazo Uturuki itasimamia ufundi zitakabidhiwa  serikali ya Thailand. Shirika la Bozankaya limepewa wadhifa wa kusimamia  ujenzi wa treni hizo.

Vatan : « Safari za treni Van-Tabriz  zaanza upya»

Safari za treni Van-Tabriz zilizokuwa simesimamishwa kwa sababu za kiusalama zimeanza upya. Safari hizo  zimeanza upya baada ya kufugwa miaka miatatu.

 Habari Zinazohusiana