Waziri Mkuu wa Uturuki azungumza kuhusu operesheni Qandil

Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım amezungumza kuhusu operesheni inayofanywa na jeshi la Uturuki Qandil.

Waziri Mkuu wa Uturuki azungumza kuhusu operesheni Qandil

Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım amezungumza kuhusu operesheni inayofanywa na jeshi la Uturuki Qandil.

Waziri huyo amesisitiza kuwa Uturuki italisafisha eneo la Qandil Kaskazini mwa Iraq dhidi ya magaidi wa KK / PYD-YPG kama ilivyofanikiwa kuukomboa mji wa Afrin nchini Syria.

Akihutubia wananchi mjini Izmir,waziri Yıldrım amesema kuwa,"Kama tulivyowaondoa magaidi Afrin kupitia operesheni ya tawi la mzaituni na kisha kuipeperusha bendera yetu,ndivyo tutakavyowasaka magaidi Qandil na kuwaangamiza".

PKK ni kundi la kigaidi linaloungwa mkono na nchi za nje kuishambulia Uturuki.

"Ni jukumu letu kuliangamiza kundi la PKK",alisema waziri huyo.

Uturuki imetangaza vita rasmi dhidi ya magaidi wanaojaribu kuikaribia mipaka yake.

Imeahidi kupambana na ugaidi.Habari Zinazohusiana