Kwanini rais Erdoğan ameshinda katika uchaguzi?

Makala ya msemaji wa ikulu ya rais mjini Ankara Ibrahim Kalın   kuhusu ushindi wa rais Recep Tayyıp Erdoğan  katika uchaguzi uliofanyika Juni  24

Kwanini rais Erdoğan ameshinda katika uchaguzi?

Makala ya  msemaji wa ikulu  mjini Ankara Ibrahim Kalın imechapishwa Juni 26 mwaka 2018  ktika jarida la Daily Sabah.

Raia wa Uturuki waliojiandikisha  kupiga kura walitimiza wajibu wao na haki yao ya kikatiba  kwa kupiga kura katika uchaguzi  mku uliofanyika nchini Uturuki Juni 24. 

Idai ya watu waliojiandikisha   kushiriki katika zoezi la kupiga kura Uturuki ilifikia asilimia 80.  Katika uchaguzi huo rais Erdoğan ameshinda katika uchaguzi kwa asilimia 52,3 ya kura. Matokeo hayo , tume ya uchaguzi imefahamisha kuwa  rais Erdoğan ameshinda kwa zaidi ya kura milioni 10   dhidi ya mgombea mwenza.

Chama cha AKP kimepata ushindi kwa 42,5. Muungano na chama cha MHP   umepata viti viti vingi bungeni.

Matokeo ya uchaguzi yanonesha wazi kuwa  Uturuki inamuamini rais Erdoğan na chama cha AKP.

 

 Habari Zinazohusiana