Rais wa Uturuki kufanya ziara nchini Zambia na Afrika Kusini

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan anatarajiwa kufanya ziara nchini Zambia na Afrika Kusini

Rais wa Uturuki kufanya ziara nchini Zambia na Afrika Kusini

 

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan anatarajiwa kufanya ziararasmi nchini Zambia na Afrika Kusini ambapo atashiriki katika mkutano  na marais  katika muungano wa BRICS . Mkutano wa BRICS utafanyika  mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini kuanzia Julai 25 hadi Julai 27. 

Baada ya kushiriki katika mkutano huo rais wa Uturuki atajielekeza nchini Zambia  Julai 28.

Katika mkutano huo rais Erdoğan atazunguza na viongozi  kuhusu ushirikiano na Uturuki.

BRICS ni muungano wa mataifa matano ambayo uchumi wake unaonekana kuwa katika ushindani mkubwa ulimwenguni nayo ni Brasil, Urusi, India, China na Afrika Kusini.

Mataifa hayo ni wanachama wa muungano wa G-20 kama  Uturuki.

Rais Erdoğan atakutana na rais wa Zambia Edgar Lungu na kuzungumza kuhusu ushirikiano baian  ya Uturuki na Zambia.

 

 



Habari Zinazohusiana