Mtoto kiziwi wa Marekani atibiwa Uturuki

Mtoto wa miaka mitatu kutoka Marekani amabaye alizaliwa bila uwezo wa kusikia, kiziwi, atibiwa na kupona Uturuki

Mtoto kiziwi wa Marekani atibiwa Uturuki

Kuhusiana na matatizo ya kutosikia, ukiziwi, ambayo baazi ya watoto huzaliwa nayo yanayotokana na hitilafu katika mfumo wa fahamu, duniani ni Uturuki pekee upasuaji mkubwa kwa ajili ya kurekebisha matatizo haya hufanyika.

Matabibu wa Kituruki wametia saini kufanya upasuaji wa matibabu zaidi.

Mjumbe wa bodi ya Wahadhiri wa chuo kikuu cha tiba cha Hacettepe (HU) cha jijini Ankara daktari bingwa wa masikio pua na koo, Profesa daktari  Levent Sennaroğlu pamoja na daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mfumo wa fahamu profesa dokta Burchak Bilginer wakiongoza timu ya wataalamu wamemfanyia upasuaji mtoto wa miaka mitatu Konor Manser anayetokea katika jimbo la Las vegas Marekani, ambaye haikuwezekana kutibiwa huko kwao hivyo basi kuletwa Uturuki, ambapo wameweza kumpatia mtoto huyo uwezo wa kusikia.

Katika maelezo yake profesa dokta Sennaroglu amesema matatizo hayo ya kusikia wanayozaliwa nayo watoto yanayotokana matatizo ya kutofanyika vizuri neva za usikivu matibabu yake ni kuweka kifaa maamlum katika sikio la ndani na kama ni neva hazijafanyika basi huwa wanapandika sehemu ya ubongo inayohusiana na kusikia tiba hizo huwawezesha watoto kusikia, na upasuaji wote hufanyika mara moja.

Matabibu wa fani tofauti hushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kuhakisha mgonjwa anapona na kupata usikivu katika masikio yote mawili alisema Sennaroglu.

"Upasuaji wa aina hizi mbili kwa mara moja unafanyika katika nchi moja tu Uturuki na hospitali moja tu Hajetepe" alisema dokta Sennaroglu.

Kwa mara moja Koklea (sikio la ndani) linapandikizwa na wakati huohup unafanyika upasuaji wa shina la ubongo, upasuaji wa aina hii wameshaufanya kwa wagonjwa watano alifahamisha Senaroglu " Katika dunia upasuaji wa aina hii umefanyika kwa mara ya sita na umefanyika hapa Uturuki katika hospitali ya Hajetepe.".Habari Zinazohusiana