Balozi mdogo wa Saudia aondoka mjini Istanbul

Mohammad al Utayb balozi mdogo wa Saudia  aondoka mjini Istanbul na kurejea nchini Saudia

Balozi mdogo wa Saudia aondoka mjini Istanbul

 

Mohammad al Utayb , balozi  mdogo wa Saudia nchini Uturuki aondoka nchini Uturuki na kurejea Saudia  kufuatia sakata la  mwanahabari Jamal Khashoggi ambae alionekana akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia  mjini Istanbul.

Kwa mara ya mwisho Khashoggi alionekana Oktoba 2.

Balozi mdogo wa Saudia  ameondoka nchini Uturuki kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Atatürk majira ya jiano Jumanne.

Kulingana  na  taarifa kutoka katika ofisi za waziri wa mambo ya nje Uturuki, Uturuki  haikuchukuwa uamuzi wowote kuhusu balozi mdogo wa Saudia.

Mohammad al Utayb hakurejea katika  makaazi yake tangu kutangazwa kupotea kwa Jamal Khashoggi Oktoba 2.

 

 Habari Zinazohusiana