"Tutaendelea kusonga mbele na  kuangamiza magaidi  Kaskazini mwa Irak"

Rais Erdoğan asema kuwa jeshi la Uturuki litaendelea kusonga mbele na kuwaangamiza magaidi Kaskazini mwa Irak

"Tutaendelea kusonga mbele na  kuangamiza magaidi  Kaskazini mwa Irak"

Recep Tayyıp Erdoğan, rais wa Uturuki amesema kuwa jeshi la Uturuki katika harakati zake za kupambana na ugaidi litaendelea kusonga mbele na kuwaangamiza magaidi  Kaskazini mwa Irak.

Jeshi la Uturuki linaendesha operesheni zake dhidi ya magaidi wanaojaribu kuweka ngome zao Kaskazini mwa Irak.

Ngome za magaidi katika milima  ya Qandil na Sinjar zitaendelea kushambulia hadi kutakaphakikishwa kuwa hakuna magaidi wanaotishi usalama Uturuki.

Rais Erdoğan ameyafahamisha hayo katika hafla ilioandaliwa ikulu katika madhimisho ya miaka 80 ya kifo cha baba wa taifa la Uturuki Mustafa Kemal Atatürk.

Katika  hafla hiyo rais Erdoğan amesema kuwa  Uturuki  ni taifa mbalo linatoa misaada ya kiutu ulimwenguni ikilinganishwa na kipato cha ndani.

Kwa upande mwingine rais Erdoğan amefahamisha vifo vya wanajeshi wanne na wengine 2 kujeruhiwa  katika ajali iliotokea Iumaa katika  ghala la silaha Hakkarı.

 Habari Zinazohusiana