Uturuki yalaani shambulizi la bomu nchini Somalia

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imelaani vikali shambulizi la bomu lililotokea katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia.

Uturuki yalaani shambulizi la bomu nchini Somalia

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imelaani vikali shambulizi la bomu lililotokea katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia.

"Tunashutumu sana ugaidi huko Mogadishu, uliofanywa na magari yaliyokuwa yametegwa bomu na kusababisha mauti na maumivu ya watu wengi.Mungu awalaze mahali pema peponi wale wote waliopoteza maisha na kuwapa shifaa majeruhi.",ilisema wizara hiyo.

Watu takriban 23 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa baada ya magari matatu kulipuka katika mji mkuu wa Somalia.

Kwa mujibu wa habari,baada ya milipuko hiyo umwagaji wa risasi ulifuatia.

Hoteli hiyo ipo karibu na makao makuu ya  idara ya uchunguzi wa wahalifu nchini humo.

Kati ya waliopoteza maisha baadhi walikuwa ni maafisa polisi na wengine raia wa kawaida.Habari Zinazohusiana