Mfanyabiashara muanzilishi wa chapa ya Crispino auawa kwa kupigwa risasi

Mfanyabiashara muanzilishi wa chapa ya Crispino,Ali Riza Gultekin, auawa kwa kupigwa risasi jijini Istanbul

Mfanyabiashara muanzilishi wa chapa ya Crispino auawa kwa kupigwa risasi

Mapema Alhamis vyanzo vya kipolisi vilisema kwamba Ali Riza Gultekin, 57, muanzilishi wa chapa ya kituruki ,Crispino, na mmiliki wa maduka mengi ya nguo za wanaume ameuawa kwa kupigwa risasi katika wilaya ya Beşiktaş jijini Istanbul.

Wavamizi wanne wenye silaha walifika katika jengo ambalo Gultekin alikuwa ameketi na marafiki zake na kufanya tukio hilo.

Mwili wake ulipelekwa mochwari baada ya uchunguzi wa kipolisi katika eneo la tukio kukamilika.

Mpaka hivi sasa polisi Istanbul imeshawatambua washukiwa na uchunguzi unaendelea kuweza kubaini mpango mzima na walioupanga.Habari Zinazohusiana