Makamu wa rais wa Uturuki kufanya ziara nchini Sudan

Fuat Oktay , makamu wa rais wa Uturuki kufanya ziara nchini Sudani

Makamu wa rais wa Uturuki kufanya ziara nchini Sudan

Makamu wa rais wa Uturuki Fuati Oktay atarajiwa kufanya ziara nchini  Sudan Jumatatu Novemba 19.

Ziara hiyo ya   makamu wa rais wa Uturuki itachukuwa muda wa siku 3.

Katika ziara yake hiyo nchini Sudan, vyanzo vya habari kutoka katika ofisi za makamu wa rais wa Uturuki mjini Anakra vimefahamisha kuwa kutazungumziwa ushirikiano uliopo kati ya Uturuki na Sudan na masuala mengine ya kimataifa.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan alifanya ziara nchini Sudan ambapo kulisainiwa makubaliano ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Fuat Oktay katika ziara yake hiyo atashirikiana na waziri wa biashara  Ruhsar Pekcan na waziri wa  kilimo na misitu Bekir Pakdemirli.

 Habari Zinazohusiana