Harakati za Uturuki kujiimarisha kiulinzi

Tarkan Zengin: Mafanikio ya kiwanda cha jeshi cha vifaru na vifaa vya kivita cha Kayseri

Harakati za Uturuki kujiimarisha kiulinzi

 

 Katika nchi ya Uturuki viwanda vya kijeshi vinachangia kwa kiasi kikubwa kukuza pato la taifa . Viwanda vya kijeshi ambavyo ni ofisi za umma vina umuhimu mkubwa kwani hutoa ajira kwa wananchi wengi. Umuhimu wake honekana zaidi hasa linapokuja suala la harakari za kijeshi na vita dhidi ya ugaidi inayoendelea nchini Uturuki.

Kurugunzi kuu ya pili ya kiwanda cha ukarabati wa vifaa vya kijeshi ilianzishwa mjini Kayser mnamo  mwaka 1951. Kiwanda hichi kilifunguliwa mwaka 1954, na kiliitwa kwa jina la Kiwanda kikuu cha ukarabati wa vifaa vya kijeshi namba 1020. Mwaka 1987 kiliitwa kwa jina la komandi yaani kiwanda kikuu cha ukarabati wa vifaa vya kijeshi namba 1009. Mwaka 2003 kikabadilishwa tena jina kikaitwa Komandi kuu ya pili ukarabati . Mwaka 2016 kilibadilishwa jina na kuitwa Kurugenzi kuu ya  2 ya kiwanda cha ukarabati, jina ambalo kimedumu nalo mpaka hivi sasa.

Katika kiwanda hichi kuna takribani wafanyakazi 800. Kati ya hao 480 ni vibarua na wengine ni maafisa wa jeshi, makuruti na maafisa wa kiraia. Uongozi pamoja na wafanyakazi wote kwa ujumla wamepata mafanikio makubwa.

 

Kiongozi wa elimu wa Türk Harb-İş Tarkan Zengin anafafanua kuhusiana na mada hii...

 

Kurugunzi kuu ya  2 ya Kiwanda cha ukarabati ni sehemu ya jeshi la  Uturuki na kazi yake ni kukarabati na kutengeneza  vifaa vya kijeshi, kubuni, kutengeneza na kuboresha  vifaa vya kijeshi, pamoja na vipuri vyake. Vifaa vya kijeshi hujumuisha; Vifaru na magari mengine ya kivita yenye silaha “Tanks, Armored Personnel Carriers , Armored Combat Vehicles , Armored Mortar ”, Kurugenzi hii pia huudumia kwa kutoa usaidizi kwa komandi nyingine zote. Kurugenzi kuu  ya 2 ya kiwanda cha ukarabati ya Kayseri pia hufanya kazi nyingine ziuatazo:

1.Hutengeneza Vipuri vya vifaa ( magari) ya kijeshi,

2.Hutengeneza Mota na mfumo usambazaji nishati wa magari haya ya kijeshi,

3. Upimaji wa vifaa vya kielektoniki na kimekanik ,

4.Kutoa elimu kwa wafanyakazi wa  nchi washirika au nchi rafiki,

5.Kutoa ushauri kwa vikosi vingine vya kijeshi.

 

VIFARU AINA YA M-60 T  VIMEUNDWA UPYA

Tangu kuanzishwa kiwanda hichi imefanya mabadiliko katika magari mengi ya kijeshi, kimefanya kazi nyingi za kuunda upya vifaa mbali mbali vya kijeshi. Kutokana na uzoefu uliopatikana kiwanda hichi kimeweza kuviboresha kuwa  vya kisasa, zaidi ya vifaru 2000  aina ya M48AT1-T2. Kiwanda hicho kimeweza kutengeneza vifaru aina ya TAMAY pamoja na vipuri vya magari mbali mbali ya kijeshi. Pia kiwanda hicho kilibadili kwa mafanikio magari ya kivita M113 ZPT kutoka kutumia mfumo wa petrol kuyafanya kutumia mfumo wa dizel. Pia kiliboresha eneo la kuhifadhia nishati kwenye magari hayo. Kiwanda hicho kimeweza kuboresha  na kuunda upya na hivyo kuboresha ufanisi wa vifaa mbali mbali vya kijeshi kama M113 A2T2.  Kiwanda hichi kilifanya kazi mbali mbali kwa hitajio la jeshi la Uturuki kama vile kuunda magari aina ya Manga. Magari ya kijeshi ya nchi kavu na magari ya zima moto. Miaka ya hivi karibuni kiwanda hiki kimeboresha vifaru aina ya M60T pamoja na kutengeneza vipuri vya vifaru aina ya MLC 70.

Katika kuboresha vifaru aina ya M60T kwa mara ya kwanza wameweza kuviongenezea mfumo wa ulinzi dhidi ya milipuko (Explosive Reactive Armour/ERA). Hilo lilienda sambamba na kufanya mabadiliko mbalimbali kwenye mfumo wa silaha na umbile zima la vifaru hivyo. Baada ya kuviboresha vifaru hivyo aina ya M60 waliongeza herufi T katika jina la vifaru hivyo kuwakilisha Uturuki yani jina jipya ni M60T. Katika maelezo mengine vifaru aina ya M-60 T vimeboreshwa katika kila eneo kulingana na matakwa ya jeshi la Uturuki. Baada ya uboreshaji wa aina zote hizo vifaru hivyo vitapa nafasi ya kujaribiwa katika mazingira ya aina mbalimbali mfano kwenye bwawa la maji kwenye miteremko na milima. Katika kurugenzi hiyo ya Ukarabati ya Kayseri miradi mingine kama ADOP-200 na Leopard 2A4 yote inahusu kuboresha vifaru vya aina mbalimbali kuvipa uwezo mkubwa zaidi, inaendelea.  

KITUO KINATOA HUDUMA KWENYE OPARESHENI ZA KIJESHI

Kurugenzi kuu namba 2  ya kiwanda cha ukarabati cha Kayseri, hukarabati na kutengeneza vifaa na vipuri mbalimbali kwa ajili ya magari ya vita yanayotumika kwenye oparesheni za kijeshi kama tawi la mzaituni iliyozinduliwa mwaka 2016 na opareshi ya Efrate iliyozinduliwa mwaka 2017. Kituo pia kina  kazi ya kubadilisha magari yaliyoharibiwa kabisa kwenye oparesheni hizo na pia kupeleka vipuri kwenye opareshini hizo. Ili kuweza kukudhi mahitaji ya oparesheni hizi kituo hichi kinafanya kazi mara mbili zaid kwa usiku na mchana. Kituo pia kimeendelea kutoa huduma tngu siku ya kwanza kwa oparesheni hizo za tawi la mzaituni na ya Efrate kwa kutuma timu ya wafanyakazi katika maeneo ya mapigano kuweza kukarabati magari ambayo yameharibiwa vibaya. Wafanyakazi wa kituo hiki wamefanya kazi kubwa sana  ya kupongezwa katika oparesheni hizi.

KITUO KIMEPEWA TUZO MBALIMBALI KWA UBORA WA KAZI

Kurugenzi kuu namba 2 ya kiwanda cha ukarabati cha Kayseri kimepewa tuzo mbalimbali za ubora wa kazi zake kama vile;  AQAP-2110 (tuzo inayotolewa na NATO baada kukidhi vigezo walivyoweka katika ubora wa vifaa vya kivita),

Kituo kilipatiwa Cheti cha Afya na Usalama wa OHSAS 18001 kinachotolewa na NATO, ambacho kinaonyesha kuwa kituo kinakubaliana na Hati ya ISS 14001 ya Mfumo wa Usimamizi wa Mazingira, ambayo inaonyesha kwamba kinafanya shughuli zake zote kwa mujibu wa sheria ya mazingira, na kwamba inakubaliana na sheria juu ya afya na usalama wa kazi.

Kituo hiki cha kazi pamoja na kutekeleza majukumu yake, kinatoa umuhimu mkubwa katika ubora wa kazi. Machi 4, 2017  kiliteuliwa kuwa mjumbe maalum wa shirika la viwango la Uturuki na Oktoba 18 mwaka 2017 kurugenzi ilikuwa ni kwanza kwa kurugenzi za kijeshi kutia saini katika harakati za viwango vya ubora wa bidhaa za ndani. Kiwanda hiki pia kimeteleuliwa kuwa ni kiwanda cha mfano cha wizara ya ulinzi ya Uturuki na kwa sababu hiyo kiwanda hicho kimepewa nyota tatu.

 

Ufafanuzi wa Tarkan Zengin kiongozi wa  Türk Harb-İş Sendikası

                           Habari Zinazohusiana