Magaidi wa PKK waendelea kushambuliwa

Magaidi wawili wa PKK wameripotiwa kuangamizwa kaskazini mwa iraq.

Magaidi wa PKK waendelea kushambuliwa

Magaidi wawili wa PKK wameripotiwa kuangamizwa kaskazini mwa iraq.

Mamlaka ya Uturuki hutumia neno "kuangamizwa",wakiashrikia kuwa magaidi wameuawa,wamekamatwa au wamejisalimisha wenyewe.

Mashambulizi ya anga yaliyofanywa katika mkoa wa Hakurk yamepelekea kuangamizwa kwa magaidi hao walipokuwa wakipanga mashambulizi katika maeneo ya Uturuki.

Waziri wa ulinzi katika ukurasa wake wa Twitter vilevile amesema kuwa ngome za magaidi hao nazo zimeangamizwa.

Mashambulizi hayo hasa yalikuwa yamewalenga magaidi wa PKK.

Ni zaidi ya miongo mitatu toka Uturuki ianzishe kampenni dhidi ya magaidi wa PKK.

Kundi la PKK linatambulika kama kundi la kigaidi na Marekani,Umoja wa Ulaya na Uturuki.Magaidi hao wamepelekea vifo vya watu karibu elfu arobaini nchini Uturuki,wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.


Tagi: Iraq , Ututuki , PKK , Magaidi

Habari Zinazohusiana