Ifahamu YTB

Shirika la kujitolea linalojihusisha na kudhamini wanafunzi wa kimataifa katika masomo ya elimu ya juu nchini Uturuki

Ifahamu YTB

 

Lengo kuu la Makala haya  ni kuyatizama mashirika mbalimbali ya kujitolea ya kituruki ambayo yametekeleza na yanaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya aina tofauti duniani kote.

 

Wiki kadhaa zilizopita tuliangazia shirika la TIKA ( Wakala wa Uturuki uratibu wa maendeleo na ushirikiano  ). Kuanzia wiki hii tutaanza kuangazia shirika la YTB (Kurugenzi ya jamii za waturuki na ndugu zao waishio nje ya nchi). Shirika hili la kujitolea nalo limetekeleza miradi mbalimbali mikubwa maeneo tofauti.

 

Shirika la YTB lilianzishwa April 6 mwaka 2010. Lengo kuu la kuanzishwa shirika hili ni kuratibu shughuli za  kimasomo kwa waturuki na wanafunzi kutoka mataifa ndugu wa Uturuki wanaosoma nje ya Uturuki, lakini pia kuratibu shughuli za kimasomo kwa wanafunzi wa kimataifa wanaosoma nchini Uturuki.

 

Kupitia kazi za shirika la YTB Uturuki imefanikiwa kuimarisha mahusiano na jamii ya waturuki waishio nje ya Uturuki lakini ia imefanikiwa kuimarisha mahusiano na mataifa rafiki ya Uturuki. Mahusiano hayo ni katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

 

Na kwa upande wa wanafunzi wa kimataifa wanaofaidika na ufadhili wa kimasomo; Hawa wameendelea kuwa mabalozi  wa kujitolea wanaoiwakilisha vizuri Uturuki karibu katika robo ya dunia nzima.

 


Tagi: Uturuki , YTB

Habari Zinazohusiana