Hadithi za Anatolia

Hadithi za Anatolia,Pamukkale

Hadithi za Anatolia

Leo katika hadithi za Anatolia

tutapitia hadithi ya Pamukkale. Pamukkale ni moja ya maeneo ambayo watalii wanaotembelea Uturuki wanapenda kuona zaidi. Mawe hayo yana rangi nyeupe iliyotokana na maji ya moto yaliyokuwa yanatoka chini kwa miaka mingi. Sakafu ya theluji-nyeupe huunda mandhari ya kuvutia pamoja na maji yamvuakatika mabwawa. Hapa tutatizama hadithi kuhusu Pamukkale. Hapo zamani sana, labda katika karne ya 14, familia iliyoishi katika eneo hilo iliishi katika misitu. Familia hio ilikuwa na binti mmoja. Binti huyo alionekana kuwa na sura mbaya sana. Hakuna mtu aliyekuwa akitaka kufanya kitu chochote na binti huyo kwa madai ya kuwa ni mbaya  na hio hali ikamplelekea binti huyo kuwa na huzuni kubwa na upweke. Mama wa wavulana waliomwona msichana huyo walikuwa wakiwaonya wana wao na kuwaambia "msijaribu kumleta binti huyo kwetu". Msichana huyo aliathiriwa na hali hiyo na hivyo kuamua kukimbia na kwenda sehemu isiyokuwa na watu.Alienda na kupanda katika mlima mrefu.Wakati akitembea katika mlima huo ghafla aliteleza na kuanguka katika moja ya mabwawa ya Pamukkale. Msichana huyo aliumia na kuvuja damu kwa wingi. Msichana huyo alilala katika bwawa hilo kutokana na majeraha aliyokuwa amepata bila ya kujua kuwa joto ndani ya maji ya bwawa lile linambadilisha hali yake.Aligeuka kuwa binti mzuri wa ajabu.

Baada ya muda kidogo,mmoja wa kijana wa mfalme wa mahala hapo alipita  na kumuona msichana amelala kutokana na majeraha aliyokuwa ameyapata.Alipomsogelea alipigwa na butwaa kuona uzuri wa msichana yule.Akambeba msichana yule na kumpeleka kwa baba yake.Madaktari wakaitwa kutibu majeraha ya binti yule.Alipopata fahamu alishangaa kuona yupo katikati ya watu waliomzingira kwa kumpenda na kumshangaa.Hajawahi kuona binadamu anamfurahia kutokana na sura yake mbaya hivyo basi hali hiyo ilimpa wasiwasi.Binti yule alimkimbilia kijana yule na kumshika mkono kutoka na mabadiliko ya mtizamo watu waliokuwa wakimuonyesha.

 . Siku chache baadae  iliwadia wakati wa majeraha yake kufunguliwa na baadae akapewa kioo ajitizame.Ghafla alipiga kelele baada ya kujiona tofauti katika kioo.Uso wake ulikuwa umebadilika na alikuwa amegeuka kuwa msichana mrembo sana.

Kijana yule akaomba ridhaa kwa baba yake amuoe msichana yule na kisha harusi ikafanyika.Hio ni siri ya maji ya Pamukkale.

 

 Kuna Hadithi nyingine ilihadithi wa katika hikaya za Ugiriki.Kulikuwa na mchungaji wa wanyama katika mmoja wa milima.Siku moja mungu Selena alikuja katika milima hiyo na kijana huyo kumuona tu alipigwa na butwaa kutokana na uzuri wake.Alikaa amemtizama mungu  yule na kusahau kuwa anapashwa kuchunga wanyama wake.Siku zilipita bila ya wanyama hao kulishwa kwani mchungaji wao hana hata habari.Maziwa yalianza kutiririka kutoka katika matiti ya wanyama hao na kutiririka katika mabwawa ya Pamukkale.Hio ndio ilikuwa sababu ya  rangi ya maji hayo kubadilika.Mpaka wa leo mandhari ya pamukkale ni ya kipekee na endapo utapata fursa ya kutembelea mabwawa hayo utajionea vivutio vya ajabu vya pamukkale na sehemu inayoizunguka.

Tukutane tena Juma lijalo kwa hikaya motomoto za Anatolia..Habari Zinazohusiana