Baada ya uchaguzi mkuu, IKBY

Uchaguzi mkuu wa eneo linaongozwa na Wakurdi, IKBY

Baada ya uchaguzi mkuu, IKBY

Zaidi ya watu milioni tatu waliojiandikisha kupiga kura katika eneo la Iraki linaloongozwa na serikali ya kikurdi,IKBY, ambalo lina idadi ya watu wanaokaribia milioni 6, mnamo siku ya jumapili tarehe 30 mwezi wa tisa walijitokeza kupigakura.

Imeripotiwa kwamba katika uchaguzi mkuu walijitokeza kupiga kura ni zaidi ya asilimia 57. Ingawa kwa ujumla tukio zima la uchaguzi liliendelea katika hali ya amani na utulivu, katika baadhi ya maeneo watu waliokuwa na silaha pamoja na kikundi cha kijeshi cha Peshmerga walikuwa chanzo cha vurugu.

Wakati vyama vya KYB na KDP kila kimoja kikimshutumu mwenziwe kwa udanganyifu, vyama vya Gorran na cha vuguvugu la kizazicha kijani vimekishutumu chama cha KYB kwa udanganyifu wakati wa uchaguzi.

Pamoja na maoni yote yaliokwishatolewa inaweza kusemwa kwa ujumla kwamba uchaguzi ulikuwa ni wa mafanikio. Katika hili msemaji wa wizara ya mambo ya nje,Hami Aksoy, alisema  

“Tumefurahishwa na tukio zima la uchaguzi ambalo limefanyika kwa amani na tunategemea kwamba matokeo ya uchaguzi huu yatakuwa ya manufaa katika hali ya kudumisha umoja na mshikamano kwa watu wa Irak”.     

 

Kutoka (Taasisi ya utafiti  wa siasa, uchumi na jamii ) SETA, Mtafiti-Mwandishi Can ACUN  anatufafanulia.

Kwa matokeo yasiyo rasmi inaonyesha chama cha KDP kimeibuka mshindi kwa kupata asilimia 45 ya kura. Huku chama cha KYB kikipoteza uchaguzi na kupata asilimia 19 ya kura. Chama cha vuguvugu la Goran kimepatasilimia 12 ya kura. Chama cha vuguvugu la kizazi kipya kikipata asilimia 8.3. Chama cha kiisalmu kimejinyakulia kati ya asilimia 5 na 7 ya kura zote zilizopigwa.huku chama  cha serdem kikipata asilimia moja ya kura.

Kwa matokeo haya yasiyo rasmi chama cha KDP kimejinyakulia ushindi mkubwa na kukipiku chama cha KYB, hivyo basi kupata nafasi kwa kushirikiana na vyama vingine vidogo kuunda serikali ya shirikisho. Wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea bunge nalo liliendelea na uchaguzi wa raisi. Kutokana na kwamba katiba ya Iraki hairuhusu mgombea wa uraisi anayetokana na Wakurdi asiwe mgombea wa pamoja wa KYB na KDP, hii imekuwa chanzo cha mgongono baina ya vyama hivi.

 

KDP walimteua Fuad Huseni kama mgombea wao wa uraisi wakati KYB wakimteua Berhem salih.Katika bunge la Irak uchaguzi wa siri wa  raundi ya pili kati ya wabunge wote 329 wabunge 272 ndio walioshiriki. Mgombea wa chama cha KYB, Berham Salih alipata kura 219 hivyo basi kuwa raisi wa awamu ya nne. Mgombea wa KDP, Fuad Huseni aliweza kupata kura 22. Katika uchaguzi wa uraisi kwa kuwa katika mzunguko wa kwanza kati ya wagombea wote saba hakuna aliyefikisha kura 220 zinazohitajika, hivyo basi uchaguzi ukaenda mzunguko wa pili. Katika mzunguko wa kwanza wa uchaguzi wa uraisi matokeo yalikuwa kama ifuatavyo; Berham Salih kura 165, Fuad Huseni kura 89, na mwanasiasa mwanamke mgombea binafsi, Sirve Abdulwahid akipata kura 18.  

Ushindi katika uchaguzi wa uraisi mgomgea wa uraisi wa chama cha KYB Berhem Salih ni dhahiri kwamba utaleta chachu katika siasa za ndani za eneo hili la IKBY. Wakati huo huo uchaguzi wa wabunge uliokipa ushindi mkubwa chama cha KDP, hivyo basi tutegemee mvutano mkubwa katika siasa za ndani za eneo hili.

Matokeo haya ya uchaguzi wa eneo hili la IKBY yataathiri pia mahusiano kati ya Uturuki na IKBY pia mapambano ya Uturuki dhidi ya ugaidi.Baada ya kura ya maoni ya kuwapatia uhuru IKBY, Serikali kuu ya Irak ilijibu vikali hasa katika maeneo waliyoshinda kama Kirkuk, na walitaka kurekebisha mahusiano yao na Uturuki. Katika upande wa uchumi chama cha KDP kitataka kuhuisha mahusiano yake na Uturuki, Katika eneo linaloongozwa na KYB ambapo Uturuki imefanya uwekezaji katika uwanja wa ndege wa Suelimani, bila shaka itatakikana uwekezaji uendelee. Inategemewa kwamba uhusiano wa Uturuki na IKBY utaimarika.

Kuhusiana mapambano ya kijeshi dhidi ya ugaidi yanayofanywa na Uturuki kaskazini mwa Irak ambako magaidi wa PKK walizuia jeshi la Uturuki lisiingie, sasa kutokana na ushindi wa chama cha KDP katika uchaguzi huu utaipa nguvu zaidi jeshi la Uturuki. Inafahamika kwamba uhusiano kati ya KYB na PKK ni mzuri wakati kati ya PKK na KDP si mzuri. Hivyo basi mahusiano kati ya Uturuki na IKBY yataimarika na vile vitisho dhidi ya Uturuki vya PKK vinaweza kuchukuliwa hatua visiendelee.

Kutokana na tukio la uchaguzi kuchukua miezi na vile serikali kuu ya Irak bado haikuwako ilisababisha matatizo mengine kwa mataifa yote haya mawili ya Uturuki pamoja na Irak. Sasa Uchaguzi umefanyika na mshindi amepatikana hii inategemewa kuimarisha usalama wa IKBY, Irak pamoja na Uturuki. Kama serikali kuu ya Iraki Itaundwa matatizo mengi ya Iraki  yatapatiwa ufumbuzi kiufanisi zaidi.

Kutoka (Taasisi ya utafiti  wa siasa, uchumi na jamii ) SETA, Mtafiti-Mwandishi Can ACUN  anatufafanulia.Habari Zinazohusiana